Saturday, March 14, 2009

ya magufuli ni ya kweli

Alikaa kimya midhili ya tembo aliyeingiwa na sisimizi puani,hakuwa na papara na kazi zake hili ni jambo ambalo linaendelea kumjengea mafanikio na ufanisi wa kazi zake katika wizara yake mhimu ambayo awali ilionekana kana kwamba asingelionekana kama mtendaji mzuri wa kazi.

ni jambo la kujivunia kwa kazi ambayo ameitenda kwa watanzania wote wanaendelea kumimina shukurani zao na pongezi kwa kwazi ambayo ameionyesha ya kishujaa,huyu ninayemzungumzia hapa ni waziri wa mifugo na uvuvi John Pmbe Magufuli,ama waweza kumwita shujaa anayepigania taifa katika kuhakikisha mali ya Tanzania haiibiwi kizembe.

Magufuli hivi karibuni alionyesha uwezo mkubwa na umakini baada ya kuikamata meli ya iliyosheheni mali kubwa yaani samaki ambao wamevuliwa na mataifa mbalimbali kama waphilipino,wachina na hata jirani zertu wake wamo.

umakini huu umepokewa kwa furaha na watanzania wote wapenda maendeleo shukurani zangu pia kama mtanzania zitamiminika kwa magufuli ambaye ni baba yetu wengine lakini swali lipo hapa? kama magufuli pekee ameweza kuwakamata hawa majangili na kuwaweka katika himaya yake kulikoni tunaendelea kupoteza muda wetu wa kuongelea mambo ya Dowans wakati huku tunawapa nafasi majangili kutuibia serikali inafanya hivyo kutufumba ili mali na haki ya Mtanzania iendelee kuibwa?.

kama ningelikuqwa kiongozi wa ngazi ya juu hii ingelikuwa kazi yangu ya kumpongeza kiongozi huyu ambye anafanya kazi kwa vitendo na sio kukaa ofisini akiwaagiza vibaraka waliopo chini yake.

Samaki ,dagaa,Papa,Sangara,Vibua na wengine wengi wametiwa katika nyavu za majangili sasa tutazamane katika sura zetu yup-i ameonyesha kusikitishwa na jambo hilo ambalo ni la kishujaa kwa Pombe magufuli?

Mawaziri wengine wanatakiwa kuiga vitu kama hivi na wakubaliane na ukweli kwamba magufuli ni kiongozi ambaye kila kukicha atakuwa bora kutokana na uwezo wake kikazi,tunashukuru kwa hilo maziwa yetu kwa hali hii yatakuwa salama, mfano ziwa Nyasa,kwa kina Nyasinta,Marcus Honors,Victoria kwa Ema kigolo, na mengine yakuwa salama bila kuwa na shaka.
kila jambo lina mwanzo na mwisho je akitoka magufuli nani ataweza kujitolea kama yeye?

No comments: