Sunday, October 26, 2008

uwezo na urembo wake


ughaibuni



Huu ni mji wa kisasa ambao wengi kama wametembelea ughaibuni hukutana na hali hii

uhai wa ni mazingira


Pamoja na maisha bora kama haya ni vyema kwa walio na maisha yaliyotulia kama mazingira haya wakawasaidia watoto yatima wakaishi katika mazingira kama haya.
JUKWAA LA WASANII

na saidi makala
KARIBU tena katika safu yako uipendayo ya Jukwa la
Wasanii,wiki hii tunaye Msanii aitwaye Besta Rweiquem
Mbaye katika ulimwengu wa muziki aliweza kujitambulisha
Zaidi na wimbo wake wa ‘Baby Boy’ ni mmoja wa wasanii ambao wameweza kuuweka juu mziki wa Bongo Fleva.

Yafuatayo ni mazungumzo yetu hivi karibuni tulipokutana ,mitaa ya Posta Jijini hili la Dar es Salaam ambapo tuliweza kuzungumza mambo mengi yanayo husu maisha yas muziki na mengine mengi kama hivi..

Bingwa:Habari za leo Besta,vipi mbona kimya kulikoni au umeachana na mambo ya muziki?

Besta:Salama,pole na kazi, muziki sijaacha kukaa kimya sio kwamba msanii anaachana na mambo ya muziki bali kuna kitu anakuwa anafanya.

Bingwa:Unataka kuniambia hadi sasa bado unatengeneza kazi au vipi hapo?mashabiki wako wangependa kujua maana wameku miss?

Besta:Nianze na hili la kazi,sasa hivi ninashughulika na kazi zangu binafsi ambazo hazihusiani na muziki na kazi hizi nazifanyia jijini Mwanza,la pili mashabiki wanakijua kipaji changu wasubiri tu kazi zangu zikipungua najua watapata uhondo wote kama ilivyokuwa awali.

Bingwa:unaweza kunijuza angalau hizo kazi ambazo unazifanya ambazo zimekufanya kukuweka wewe bize kiasi cha kuwanyima mashabiki haki zao hasa wale ambao walikuwa karibu na wewe kisanaa?.

Besta:ndio maana hapo awali nimesema kuwa kazi au mambo ya binafsi kwa hilo utanisamehe(Kicheko).

Bingwa:Mwaka unaelekea ukingoni sijui kuna kitu chochote ambacho umekiandaa kwa ajili ya kuaga mwaka au hiyo ndio itoke hadi mwaka 2010 kama mungu atakuweka hai?

Besta:Hilo sijaliwaza kabisa mimi ni msanii naweza kutengeneza kazi wakati wowote lakini kama nilivyosema kuwa nimetingwa na majukumu sana sina budi kuyamaliza kwanza ndipo hapo baadaye nijue kinachofuata.

Bingwa:Dah!inaonekana kazi kweli zimekutinga.ok tuachane na mabo ya muziki,kwa ujumla naomba tuangalie mambo mengine.

Bingwa:Kando ya muziki vitu gani ambavyo wewe unavipenda na unavyojishughulisha navyo wakati ukiwa umepumzika?

Besta:kuna mambo mengi ambayo nayapenda ,tofauti na muziki lakini katika kazi za kujishughulisha nazo zipo nyingi si unajua kazi ni kazi yoyote ambayo nitajua hii uinaniingizia kipato nafanya.

Bingwa:mchezo gani ambao unaupenda kando ya muziki?

Besta:Sanaa ndio kitu ambacho kimeshikilia maisha yangu tangu nikiwa mtoto nadhani nilikuwa napenda hivyo si dhani kama kuna mchezo ambao unaingia akilini mwangu kama muziki.

Bingwa:Unauonaje muziki wa kizazi kipya ulivyo kwa sasa kuna madai kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanaonekana kuuvamia muziki?

Besta:Kwa kweli hilo mimi siwezi kusema muziki umevamiwa maana nikisema hivyo nitakuwa siwatendei haki wasanii wote ambao wanaimba hasa wale ambao wanaibukia,na kama nikisema hivyo je mimi wakati naingia katika ‘Gemu’wasanii walionitangulia na wao si wangesema nimevamia?

Bingwa:Hapo kweli.ok Mashabiki nasikia wanakuita Shakila kwanini shakila ?au wewe ndio ulipenda jina hilo.

Besta:(Kicheko) bwana hao ni mashabiki tu wameniita hivyo mimni jina langu ni Besta tu wala hakuna lingine.

Bingwa:Una siri gani kubwa ya mafanikio yako maana inaonekana wasanii chipukizi wanapenda kukutolea mfano kuwa wawe kama wewe,wakati huo huo tukiangalia hausikiki katika jukwaa?

Besta:Hivi unajua utulivu ni kitu mhimu maishani huenda kutokana na mimi wanavyoona nipo kimya bila ugomvi na msanii yoyote wanavutiwa nami lakini zaidi huwezi kujua kwa nini watu wanavutika nami sijui kwa kweli nisiseme uongo

Bingwa:Swali la kifamilia je umeolewa au mchumba,au bado upo upo kwanza?

Besta:(kicheko kikubwa) Unatakakunioa nini mtu wangu ! sijui nisemeje maana hili swali huwa nakutana sana nalo lakini bwana fanya hilo liwe chini ya kapeti (siri) yetu wa wili maana si vizuri kuliongelea sana jambo hilo au sio.

Bingwa:Poa isiwe tatizo,tuachane na jambo hilo labda wapenzi na mashabiki wako kwa ujumla wategemee nini mwishoni mwa mwaka huu au mwakani?

Besta:Mimi ni msanii,mashabiki najua wameni mis kweli lakini nitakuja nitafuta kila kosa na watafurahi sana ila siwezi kuambia ni mwaka huu au hadi mwakani maana najua kazi ya kuimba ni jukumu langu.

Bingwa:tukitoka nje ya nchi tunaona wasanii wengi wanafanya vizuri katika soka la muziki hata kimauzo unadhani kitu gani kina fanya soko la hapa nyumbani kuwa chini hivyo?

Besta:Swali zuri sana unajua kazi zetu tunazifanya kwa makini sana lakini wizi ni mkubwa sana pindi kazi inapokuwa sokoni kuna watu wa janja sana wanapenda kula kupitia sisi sasa unakuta kazi ni nzuri lakini msanii analalamika mauzo ni madogo,alafu kitu kingine wasanii wetu waliowengi wanajisikia wamefika ukiwaangalia shule ni ndogo kuimba nako wanafanya kwa kutegea kwa hiyo huwezi kushindana na msanii msomi kama wale wan chi za wenzetu.

Bingwa:Unaposema wasomi unamaanisha wasanii wetu wana elimu ndogo au iko vipi hiyo wapenzi na mashabiki wa muziki wangependa kujua juu ya hilo?

Besta:Hilo bwana lipo wazi wala halina ubishi atakaye kataa ni mbishi tu wasanii wengi ukiwaangalia na kuwauliza wengi wao utakuta wameishia kidato cha nne au kasoma sana kidato cha sita lakini asilimia kubwa hakuna elimu na elimu sio lazima iwe ya vidato tu la! kuna elimu za sanaa na kujiendeleza sasa wengine ndio unakuta hata kumaliza kidato cha nne hawajamaliza wanataka mafanikio makubwa sijui, lakini kwa wengine watasema vipi kuhusu hilo lakini sisi hatuwezi kufanya vizuri zaidi kimuziki ndio maana unaona mtu kama mimi naona heri nipumzike kidogo kufaya vitu vingine ambavyo nimevisomea kuepukana na wizi wa kazi zetu.

Bingwa:Kwa hiyo huenda hilo ndio jambo kubwa ambalo limekufanya wewe ukae kimya kiasi hicho,na tofauti na hivyo wewe juzi tu umemaliza chuo nchini Uganda sasa inakuwa vipi unashindwa kuendelea kusonga mbele, na muziki kwa sababu elimu tayari unayo ya kutosha ili uweze kupigana na soko nje ya nchi?

Besta:Mmmh! Kaka mimi kazi ya muziki kama nilivyokueleza hapo awali naipenda najua kuwa hicho ni kipaji changu siogopi hali hiyo, lakini ukiangalia kwa makini na ukafikiri sana muziki sio wa maisha na sio wa kuutegemea sana,kuhusu kusoma kwangu ni sehemu ya maisha ya kila binadamu sijuyi nasijafikiria kutoka kimuziki nje ya nchi maana nimeona majukumu mengi yananibana.

Bingwa:Besta kweli wewe unaweza kuangalia mbali,sasa hivi umehamia mjini Mwanza je hiyo ni dalili ya kuhamishia makao yako huko na kuondoka kabisa jijini Dar es Salaam pakoje hapo?

Besta:ni kwelib nipo Mwanza huko naendelea na kazi zangu za maendeleo yangu.

Bingwa:Unawaambia nini wasanii ambao wanaingia kwa kasi katika ‘gemu’ na nini ushauri wako?

Besta:wawe na bidii waendelee kuuboresha muziki huu wajue kazi ipo na kuna ushindani mkubwa hasa hawa wanaoingia sasa hivi waje na mbinu mpya ambayo itakuwa na mtazamo mpya kwa mashabiki.

Bingwa:mimi nashukuru kwa ushirikiano wako na samahani kwa kukupotezea muda wako huu.

Besta:Kaka usihofu hiyon ni kazi yako nami nashukuru nakutakia kazi njema yenye mafanikio.

Huyo alikuwa ni Mwanadada kipenzi cha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya ambaye huwateka mashabiki wengi hasa akiwa jukwaani kutokana na uwezo wake wa kukata mauno kiasi cha kubatizwa jina la Shakila,akifananishwa na msanii toka nchini venizuela.

Nakutakia siku njema ya kazi mpenzi msomaji wa safu hii maridhawa tumwombe mwezi Mungu atusaidie tuweze kukutana wiki ijayo.

Kwa maoni zaidi tuwasiliane kwanjia hii hapa chini
Sammakala49@yahoo.com
0713507869

Kocha mkuu wa timu ya Tanzania 'taifa stars' Marcio Maximo ni moja ya makocha ambao sasa hivi kila nchi inatamani aweze kwenda kufundisha kutoka na uwezo wake mkubwa wa kufundisha hapa akiwa na mdau alipokuwa kazini Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Saturday, October 25, 2008


muziki kazi

kwa niaba yangu na wapenzi wa blog hii naomba maoni yenu kuhusu muziki wa bongo fleva je vijana wanapotea ama kazi inazidi kukolea

hilo ni pozi hajasinzia

besta akiwa katika pozi ,kwa sasa besta amekaa kimya kwa ajili ya kujipanga zaidi.

besta sijajua lini nitaolewa

huyo dada umwemwona akipanda jukwaani unaweza kusema kuwa siye jinsi anavyojua kulimiliki jukwaa anitwa Besta,wanamwita kiuno bila mfupa