Saturday, January 23, 2010

WALIOWENGI WANASEMA KUWA MTI UKIWA MKAVU UNA NINI..............?


HAPA! KAZI KAKA
Kwa kila jambo lilolo jema huwa na magumu sasa jiandae kuwa na maema pia ukutane na yaliyo magum karibu katika mwak huu Sijui dada yangu aliyoko Norway yupo maana amekaa kimya sana kama kwao walivyokaa sana kimya kule kunako na dagaa wazuri yaani ziwa Nyasa He! naomba ujitokeze we mama.


Haya ni majadiliano ya Nini Wadau? maana kulia ni Kocha Mkuu wa SimbaPatrick Phiri na katikakati ni Mh.Waziri wa kazi na Maendeleo ya Vijana Juma Kapuya na wa mwisho ni mkereketwa wa Simba wakimsikiliza akimwaga porojo

Mshambuliaji wa timu ya Simba Mussa Hassan 'Mgosi' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa timu ya Prisons ya Mbeya jana Laurian Mpalile katika mchezo wa jana uliofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.Mchezo huo ulimalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1


"Nashukuru umekuwa kocha pekee ulioonyesha uwezo wa kufundisha hapa nchini kwa kweli mimi naipenda sana Simba hasa hivi unavyoshinda kila mchezo tena umeweka historia ya pekee itabidi nikae nikufikirie nikupe jimbo" Hivi ndivyo inavyoonekana akisema Waziri wa Kazi na maendeleo ya Vijana Juma Athuman Kapuya jana wakati Simba ilipokuwa ikicheza na Prisons ya Mbeya ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

hizi zilikuwa za jana wakti Simba ilipotoa kipigo kwa Prisons ya Mbeya

Wadau wa soka wakijadiliana jana katika mchezo wa Simba na Prisons ya Mbeya ambapo Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 Mdau Mkuu anayeamini anaipenda Simba Mh.Juma Kapuya akilonga na jamaa ambye jina lake halikufahamika .

watoto eeehe! mzunguko huo!

Watoto wa shule ya awali ya Galomba iliyopo Keko Michungwani Dar es Salaam, wakiwa katika mchezo. Michezo kama hii kwa watoto ni muhimu kwa ajili ya kujenga afya zao na kuwajenga kiakili zaidi.

Pole Essien wa Taswa..

Kutokana na beki mahiri wa timu ya Taswa Fc Ernest Mbozi kuvunjia mguu wakati akiwa katika mechi ya kirafiki na timu yake ya Chuo, sasa atakuwa nje kwa muda usiopungua wiki 6.